1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Haki za binadamu zisihatarishwe

10 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFYJ

Wataalamu wa masuala ya usalama wanaokutana katika mji mkuu wa Hispania,Madrid wamesema Umoja wa Mataifa unahitaji kuhusishwa zaidi katika vita dhidi ya ugaidi.Wanasiasa na wataalamu kutoka zaidi ya nchi 50 wanakutana Madrid kutafuta njia ya kupambana na ugaidi bila ya kuhatarisha haki za binadamu.