1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Utawala wa sheriaIsrael

Madaktari Israel wagoma baada ya Bunge kupitisha sheria tata

25 Julai 2023

Maelfu ya madaktari nchini Israel wamegoma leo, huku viongozi wa shirikisho la wafanyakazi wakitishia mgomo mkubwa, ikiwa ni siku moja baada ya bunge kuidhinisha sheria inayodhoofisha mahakama ya juu nchini humo.

https://p.dw.com/p/4UNPN
Israel | Justizreform | Protest
Picha: MENAHEM KAHANA/AFP

Magazeti manne mashuhuri nchini humo leo yaliandika kurasa zao za mbele kwa wino mweusi, picha ya kutisha iliyolipiwa na muungano wa kampuni za teknolojia ya hali ya juu.

Maneno ya pekee katika kurasa hizoyaliandikwa chini katika mstari na kusoma "siku nyeusi kwa demokrasia ya Israel."

Soma pia:Bunge la Israel lapitisha sheria tata ya mageuzi ya mahakama

Kura ya jana Jumatatu bungeni, ambayo ni ya kwanza katika mfululizo wa hatua zinazojumuisha marekebisho ya kimahakama ya serikali ya Benjamin Netanyahu, imesababisha hisia kali kote nchini humo.