1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Bunge la Israel kupigia kura mageuzi yanayoleta mgawanyiko

24 Julai 2023

Wakati maandamano makubwa yakiendelea kufukuta katika miji mikubwa na ya kimkakati kupinga marekebisho yenye utata ya mfumo wa mahakama, bunge linatarajiwa kupiga kura baada ya majadiliano ya usiku kucha.

https://p.dw.com/p/4UJP9
Israel | Proteste gegen Justizreform
Picha: MENAHEM KAHANA/AFP/Getty Images

Hii ni hata baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kuhimiza kuahirishwa kwa mswaada huo uliosababisha mgawanyiko na miezi kadhaa ya maandamano ya umma.

Wabunge walijadili usiku kucha wakati kukiwa na juhudi za mwisho mwisho za Rais Isaac Herzog kufikia maelewano.

Alikutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu katika hospitali alikofanyiwa upasuaji wa moyo.

Soma pia:Hotuba ya Netanyahu yaibua maandamano mapya Israel

Netanyahu aliruhusiwa kuondoka hospitali leo na tayari yuko bungeni kwa ajili ya mchakato wa upigaji kura.

Polisi leo wametumia mizinga ya maji ya kuwashakuwatawanya waandamanaji waliofunga lango la bunge.

Wakosoaji wanahofia kuwa mabadiliko ya mfumo wa mahakama yatadhoofisha demokrasia ya Israel.

Sheria hiyo inayopendekezwa itaupunguza uwezo wa majaji kuyakataa maamuzi ya serikali wanayoyaona kuwa hayafai.