1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron atarajiwa kuwaondoa wanajeshi wake Mali

16 Februari 2022

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kutangaza rasmi dhamira yake kwamba wanajeshi wa nchi yake walioko Mali waondolewe na wapelekwe kwingineko katika kanda hiyo ya Sahel.

https://p.dw.com/p/475uV
Frankreich | G5 Gipfel | Präsident Emmanuel Macron
Picha: Blondet Eliot/ABACA/picture alliance

Duru za kidiplomasia zimeeleza hayo baada ya Macron kukutana na viongozi wa ngazi ya juu kutoka kanda ya Sahel Jumatano. 

Kulingana na vyanzo vya habari, hatua inayotarajiwa ya Macron inafuatia kuvunjika kwa uhusiano kati ya Ufaransa na utawala wa kijeshi wa Mali.

Mali yampa balozi wa Ufaransa saa 72 kuondoka nchini humo

Duru kadhaa za usalama ambazo hazikutaka kutambulishwa zimelielezea shirika la habari la AFP kwamba tangazo la Macron litakalomaliza miaka tisa ya ujumbe wa Ufaransa nchini Mali, litajiri wakati sawa na mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika utakaofanyika Brussels Alhamisi na Ijumaa.

Kwa Ufaransa, kuwaondolea wanajeshi wake Mali ni badiliko la kimkakati, kufuatia mapinduzi mawili ya kijeshi lakini hasa kufuatia kuvunjika kwa uhusiano na taifa hilo ambalo ni koloni lake la zamani na pia Rafiki.

Mnamo mwaka 2013, Ufaransa ilivituma vikosi vyake nchini Mali kupambana na wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu kaskazini mwa Mali.
Mnamo mwaka 2013, Ufaransa ilivituma vikosi vyake nchini Mali kupambana na wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu kaskazini mwa Mali.Picha: Christophe Petit Tesson/Pool/abaca/picture alliance

Je, ndio mwisho wa ujumbe wa Ufaransa nchini Mali?

Hatua hiyo itatia kikomo ujumbe wa Ufaransa ambao marais wake wa zamani waliutaja kuwa muhimu kwa usalama wa kanda hiyo na Ulaya.

Vikosi vya Ufaransa vyamuuwa mkuu wa IS ukanda wa Sahel

Mnamo Jumatatu, waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian alisema kupitia taarifa kwamba ikiwa mazingira nchini Mali hayawezeshi operesheni za vikosi vyao- jambo ambalo ni bayana, basi wataendelea kupambana na ugaidi lakini kwa ushirikiano na nchi nyingine katika kanda hiyo.

Rais wa Mali na Waziri Mkuu washikiliwa na jeshi

Duru za kidiplomasia zimeeleza kwamba Macron pia anatarajiwa kukutana na wakuu wa nchi za Afrika kutoka kanda hiyo Jumatano, kuelekea mkutano wa kilele unaoanza Alhamisi hadi Ijumaa kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.

Huku uchaguzi wa urais nchini Ufaransa ukitarajiwa mwezi Aprili, Macron hataki taswira mbaya kujitokeza kama iliyovyokuwa kwa Biden wakati Marekani ilipowaondoa wanajeshi wake Afghanistan mwaka uliopita, au ishara yoyote kwamba hakuna cha kujivunia katika uwepo wa wanajeshi wake Mali ambapo 48 wameshauawa hadi sasa.

Mwenyekiti wa ECOWAS asema mapinduzi ya Mali yalikuwa yanaambukiza

Mapinduzi mawili ya kijeshi Mali

Duru za kidiplomasia zimeeleza kwamba Macron pia anatarajiwa kukutana na wakuu wa nchi za Afrika kutoka kanda hiyo Jumatano, kuelekea mkutano wa kilele unaoanza Alhamisi hadi Ijumaa kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.
Duru za kidiplomasia zimeeleza kwamba Macron pia anatarajiwa kukutana na wakuu wa nchi za Afrika kutoka kanda hiyo Jumatano, kuelekea mkutano wa kilele unaoanza Alhamisi hadi Ijumaa kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.Picha: Stephane de Sakutin/AP Photo/picture alliance

Baada ya mapinduzi mawili nchini Mali tangu mwaka 2020, Ufaransa na nchi nyingine za magharibi zililalamika kwamba jeshi limeshindwa kurejesha utawala wa kiraia kulingana na muda uliokubaliwa. Badala yake jeshi limezidi kuwa na uhasama dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa na wa Ulaya walioko nchini humo.

Hayo yanajiri huku Mali ikiimarisha urafiki na Urusi, na kushirikiana na mamluki wanaoshukiwa kuwa wanajeshi binafsi wa Urusi kutoka kampuni ya Wagner.

 Mashambulizi ya wanamgambo yaibua wasiwasi

Katika miezi ya hivi karibuni, mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya nchi za kusini mwa Mali, yamezusha hofu kwamba wanamgambo hao wanasogelea ghuba ya Guinea.

Macron ambaye tayari alinuia kupunguza idadi ya wanajeshi hao wanaokaribia 5,000, sasa anatarajiwa kuwapeleka katika kambi zao zilizoko nchi jirani mfano Niger.

Mnamo mwaka 2013, Ufaransa ilivituma vikosi vyake nchini Mali kupambana na wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu kaskazini mwa Mali.

(Afpe, Rtre)