1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron asema tukio la polisi kumuuwa kijana halikubaliki

28 Juni 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameelezea tukio la polisi kumuuwa kwa kupigwa risasi kijana mwenye umri wa miaka 17 katika kituo cha ukaguzi wa barabarani karibu na mji mkuu Paris, kuwa kisichokubalika.

https://p.dw.com/p/4TBXC

Rais Emmanuel Macron amewaambia waandishi habari mjini Marseille kuwa hakuna kinachohalalisha kifo cha kijana mdogo.

Ametoa wito kwa idara ya mahakama kufanya kazi yake. Afisa mmoja wa polisi anachunguzwa kwa mashitaka ya kuuwa bila kukusudia kwa kumpiga risasi kijana huyo.

Jirani yake alisema kijana huyo ni wa kutoka familia ya Kialgeria. Waendesha mashitaka wamesema alikataa kushirikiana na polisi alipoamriwa kusimamisha gari lake Jumatatu asubuhi.

Wizara ya mambo ya ndani imetoa wito wa utulivu baada ya watu 31 kukamatwa katika vurugu za usiku kucha, hasa katika kitongoji cha Nanterre cha mji mkuu Paris ambako muhanga huyo aliishi.

Mashirika ya haki yanadai kuwepo ubaguzi wa rangi wa kimfumo katika taasisi za utekelezaji wa sheria nchini Ufaransa, madai ambayo Macron aliyakanusha.