Machafuko yaendelea Senegal yakishinikiza uchaguzi
14 Februari 2024Matangazo
Hatua ya Rais Macky Sall ya kuahirisha uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 25 hadi mwezi Disemba, imeitumbukiza Senegal kwenye mgogoro mbaya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuambia utawala wa Senegal kuwa ni muhimu na ni haki ya Wasenegal wote kuheshimiwa pale wanapokusanyika kueleza hisia zao kwa amani.
Soma pia:Uchumi wa Senegal kuzorota kutokana na mkwamo wa kisiasa
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema Guterres ametoa wito wa kutatuliwa mgogoro wa Senegal kwa njia zilizowekwa za kikatiba.
Ufaransa ambayo ni mkoloni wa zamani wa taifa hilo la Afrika Magharibi ameitaka Senegal ihakikishe inatoa majibu sahihi kuhusiana na maandamano na imetaka kura ya rais ifanyike haraka iwezekanavyo.