1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maaskofu waonya kuhusu kucheleweshwa uchaguzi DRC

Jean Noel Ba-Mweze2 Machi 2021

Mkutano wa Kitaifa wa Maaskofu wa Kongo (CENCO) umeonya kuwa raia hawatavumilia uchaguzi kuahirishwa. Uchaguzi mkuu unatarajiwa nchini humo mwishoni mwa mwaka 2023, lakini hakuna ishara yoyote katika mwelekeo huo.

https://p.dw.com/p/3q6U1
Kongo Donatien Nsholé, Generalsekretär Cenco & Jean Marie Bomengola, Sprecher
Picha: DW/W. Bashi

Uchaguzi mkuu unatarajiwa nchini humo mwishoni mwa mwaka 2023, mwaka ambao huenda ukapita bila chochote kufanyika kutokana na hali ya mashaka inayoendelea kushuhudiwa, na picha ya huzuni iliyotafsiriwa na maaskofu wa Kanisa Katoliki.

"Hakutakuwa na udhuru wa kutofanya uchaguzi mkuu uliopangwa hapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 2023 ujao," walitilia mkazo maaskofu hao katika ujumbe uliopewa kichwa: "Rarua moyo wako na sio nguo zako, watu bado wanasubiri".

Kwa mjibu wa maaskofu hao, kuna pengo kubwa kati ya ahadi kutoka mamlaka na ukweli hapa nyumbani, na wananchi wanaishi katika hali isiyo na uhakika.

Kongo Notre-Dame in Kinshasa
Kanisa Katoliki ni miongozi mwa taasisi zenye ushawishi mkubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.Picha: picture-alliance/dpa/N. Bothma

Soma pia: Kinshasa: Waandamanaji wawili wauawa kwa kupigwa risasi
 

"Serikali ifanye marekebisho ya uchaguzi kuwa moja ya vipaumbele, ili kuboresha usimamizi wa uchaguzi na kuimarisha demokrasia," alisema padri Donatien Tshole, katibumkuu wa CENCO.

Ameitaka serikali kufanya kila liwezekanalo ili kuandaa uchaguzi wa kuaminika, ulio wazi, na wa amani mnamo mwaka 2023 na sio baadaye.

DR Kongo Präsident Kabila einigt sich mit Opposition Felix Tshisekedi
Rais wa Congo Felix Tshisekedi.Picha: Reuters/K. Katombe

Tume ya uchaguzi yaungana na Maaskofu

Kwa upande wake, kiongozi wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) Corneille Nangaa ametoa mwito kwa serikali kuwa tayari kuandaa uchaguzi huo wa 2023, na kusema kwamba hilo ndiyo litaepusha kucheleweshwa uchaguzi kama ilivyotokea 2016.
Soma pia: Asasi za kiraia zalia na hitilafu uchaguzi DRC

"Nawaomba viongozi wasisubiri kuzindua maandalizi ya uchaguzi huu, pamoja na kuwekwa kwa viongozi wapya watakaochukua nafasi yetu. Kuanzisha mageuzi ya kweli ambayo hayatapingana na utayarishaji wa uchaguzi ujao."

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inapaswa kuandaa kwa wakati mmoja, uchaguzi wa rais, wabunge, manispaa na mitaa.