1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa DRC huenda usifanyike Jumapili

Sekione Kitojo
20 Desemba 2018

Uchaguzi wa rais unaosubiriwa kwa hamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huenda usifanyike Jumapili, baada ya tume ya uchaguzi kuwaambia wagombea leo kuwa haiwezi kuandaa zoezi hilo kwa wakati unaofaa.

https://p.dw.com/p/3AS6v
Demokratischen Republik Kongo | Wahlkommision |  Corneille Nangaa
Picha: DW/F. Quenum

Tume  ya  uchaguzi  katika  Jamhuri  ya  kidemokrasi  ya Congo  imesema  uchaguzi  uliopangwa  kufanyika  siku  ya Jumapili  hautafanyika  na  inatoa  wito  wa  kuahirishwa.

Afisa  kutoka  upinzani  Jacquemin Shabani  ameliambia shirika  la  habari  la  Ujerumani  dpa  kuwa  uchaguzi hautafanyika, na  kwamba  hivyo  ndio   rais  wa  tume  ya uchaguzi alivyowaambia.

Anaomba  uchaguzi  huo  uahirishwe, amesema  Shabani, afisa  kutoka  chama  cha  mgombea  wa  kiti  cha  urais katika  uchaguzi  huo  Felix Tshisekedi. Uchaguzi  huo tayari  ulicheleweshwa  kwa  miaka  miwili  na  rais Joseph Kabila, ambaye  yuko  madarakani  kwa  miaka  17  sasa.

Mgombea  wa  chama  tawala  cha  rais  kabila  Emmanuel Ramazani  Shadary  anapambana  na  wagombea  wawili wa  upinzani , Tshisekedi  na  martin Fayulu.