1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maamuzi ya VAR kufafanuliwa kwa mashabiki katika Euro 2024

13 Juni 2024

Maamuzi ya marefa wasaidizi wa video au - VAR yataoneshwa kwa upana zaidi katika mashindano ya kandanda ya ubingwa wa Ulaya, Euro 2024 ili kutoa uwazi zaidi kwa mashabiki na vyombo vya habari.

https://p.dw.com/p/4gzDw
Maamuzi ya VAR kufafanuliwa kwa mashabiki viwanjani katika mashindano ya Euro
Maamuzi ya VAR kufafanuliwa kwa mashabiki viwanjani katika mashindano ya EuroPicha: Jane Stokes/Pro Sports Images/IMAGO

Maelezo ya kiufundi ya maamuzi yanayofanywa nje ya uwanja yataoneshwa kwenye skrini kubwa ndani ya viwanja na yatatolewa kwa kampuni zinazorusha matangazo moja kwa moja ili kuelewa haraka sababu au mantiki inayozingatiwa katika kila uamuzi.

Kwa mfano, badala ya kuonesha kuwa penalti ilitolewa kwa kuunawa mpira, maelezo yataonesha ni mchezaji yupi, mkono upi, na kwa nini alikokuwa mchezaji huyo kunahalalisha kutolewa penalti hiyo.

Mabadiliko haya ya kuwepo mchakato wa uwazi zaidi yaliainishwa jana mjini Munich na meneja mkurugenzi wa marefa wa UEFA Roberto Rosetti.

Michuano ya UEFA Euro 2024 inang'oa nanga kesho jioni hapa Ujerumani kwa mechi ya Kundi A kati ya wenyeji Ujerumani na Scotland.