1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Habeck: Euro 2024 ni zawadi kwa Ujerumani

10 Juni 2024

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani, Robert Habeck amesema nchi yake iko tayari kutumia fursa ya kuandaa michuano ya Kombe la Ulaya mwaka 2024 kama zawadi baada ya miaka minne migumu.

https://p.dw.com/p/4gsLl
EURO 2024 Frankfurt |
Michuano ya Euro 2024 inafanyika katika miji 10 ya nchini Ujerumani Picha: Michael Bihlmayer/CHROMORANGE/picture alliance

Akizungumza na gazeti la michezo la Kicker, Habeck amesema nafasi ya Ujerumani kuandaa michuano ya EURO 2024 ni nafasi nzuri ya kujiliwaza baada ya janga la UVIKO na mzozo wa nishati na uchumi uliosababishwa na vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Habeck amekiri kwamba mashindano hayo ya kandanda yanafanyika wakati Ujerumani ikiendelea kukabiliana na changamoto nyingi lakini kwa miaka miwili sasa imeweza kuzidhibiti.

Aliongeza kuwa nchi inastahili kuwa na "wiki nne za furaha" wakati michuano hiyo na anatumai hali hii itachochea ukuaji wa hata angalau asimilia 0.1 zaidi ya uchumi.