1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wawawekea vikwazo maafisa zaidi wa Iran

23 Januari 2023

Mawaziri wa kigeni wa Umoja wa Ulaya wapitisha duru ya nne ya vikwazo dhidi ya Iran vigiwagusa maafisa wa ngazi za juu wa Iran akiwemo waziri wake wa michezo na masuala ya vijana.

https://p.dw.com/p/4MbBy
Belgien | EU Flaggen in Brüssel
Picha: Kenzo Tribouillard/AFP/Getty Images

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani na Ufaransa wamesisitiza   juu ya umuhimu wa kuipatia msaada zaidi wa fedha Ukraine ili kuisadia katika juhudi zake za kuikabili Urusi kwenye uwanja wa vita. Kadhalika mawaziri wa kigeni wa Umoja wa Ulaya wamepitisha vikwazo dhidi ya maafisa chungunzima wa Iran.

Frankreich | Außenministerin Annalena Baerbock und Catherine Colonna
Picha: Christophe Petit Tesson/AP/picture alliance

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baebock na mwenzake wa Ufaransa  Catherine Colonna,wamesisitiza umuhimu wa kuipatia msaada mwingine wa ziada wa kifedha Ukraine kuisadia kwenye mapambano yake dhidi ya Urusi.

''Ikiwa Ukraine itashindwa vita hii, nchi hiyo haitokuweko tena na hiyo ndiyo sababu kwanini ni muhimu kwetu sisi washirika wa kimataifa kufanya tuwezalo kuisadia Ukraine katika haki yake ya kujilinda''

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani hata hivyo amekataa kutowa tamko lolote kuhusu ikiwa Ujerumani itakubali kupeleka vifaru vyake vya  kivita chapa Leopard nambari 2.Ingawa jana Jumapili alisema Ujerumani itairuhusu Poland kupeleka Ukraine  vifaru hivyo vyenye uwezo mkubwa,ikiwa nchi hiyo itaomba ridhaa ya kutaka kufanya hivyo.Ufaransa imesema haina mashaka kwamba viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels wataidhinisha sehemu ya msaada wa ziada wa fedha kwa ajili ya Ukraine.

Belgien | Treffen der EU Außenminister in Brüssel
Picha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Ama kuhusu Iran mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 27 wanachama wa Umoja huo wa Ulaya wamepitisha vikwazo dhidi ya maafisa chungunzima wa Iran wanaotuhumiwa kuwa na dhima katika ukandamizaji wa waandamanaji.Miongoni waliowekewa vikwazo ni waziri michezo na masuala ya vijana Hamid Sajjad ambaye amepigwa marufuku kusafiri nchini za Umoja huo na mali zake kuzuiwa.

Ulaya kuiwekea Iran vikwazo vipya kutokana na ukandamizaji wa maandamanoMagavana wa mikoa na wabunge ni miongoni pia mwa waliowekewa vikwazo.Hata hivyo Umoja huo umeweka wazi kwamba hautoliorodhesha jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Iran katika orodha yake ya  makundi ya kigaidi. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema vikwazo dhidi ya serikali ya Iran ni muhimu kukabiliana na ukiukaji wa haki za binadamu.

''Bado tunashuhudia nchini Iran utawala ukifanya ukatili dhidi ya wananchi wake. Utawala wa Iran,jeshi la walinzi wa mapinduzi wanawahangaisha wananchi wao wenyewe siku baada ya siku''

Tayari Umoja wa Ulaya ulishaweka mara tatu vikwazo dhidi ya maafisa wa Iran na taasisi zake wakiwamo mawaziri wa serikali,maafisa wa kijeshi na polisi ya kusimamia maadili ya nchi hiyo kutokana na ukiukaji wa haki za binadamu ulioshuhudiwa baada ya kuzukaa maandamano ya kupinga kifo cha msichana Mahsa Amini aliyekufa mikononi mwa uangalizi wa  polisi hao.

EU foreign affairs ministers meeting
Picha: Mario Salerno/European Union

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya pia wanatarajiwa kutoa idhini rasmi kwa ujumbe mpya unaosimamia suala la amani kati ya Armenia na Azerbaijan.Lakini pia watajadili hali ya usalama katika kanda ya Sahel,Afrika Kaskazini,hali ya kibinadamu Afghanistan na namna ya kuishughulikia Venezuela baada ya chaguzi za hivi karibuni huko Brazil na Colombia.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW