1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya kuiwekea Iran vikwazo vipya kutokana na maandamano

23 Januari 2023

Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa Jumatatu kutangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran.

https://p.dw.com/p/4MZjd
Frankreich Iranische Demonstrationen in Straßburg
Picha: DW

Shirika la habari la Ujerumani DPA limesema vikwazo hivyo vipya vitalenga dazeni tatu za watu binafsi na mashirika nchini Iran.

Hatua hiyo itakuwa duru ya nne ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya tangu kuzuka kwa maandamano ya kitaifa baada ya mwanamke wa Kikurdi Jina Mahsa Amini kufariki akiwa mikononi mwa polisi ya maadili mwaka jana.

Wiki iliyopita, wabunge wa Bunge la Ulaya walipiga kura kujumuishwa kwa kikosi cha walinzi wa mapinduzi ya Iran kwenye orodha yake ya ugaidi kutokana na ukandamizaji wa waandamanaji na kuiuzia Urusi ndege zisizoruka na rubani.

Hata hivyo, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema uamuzi wowote wa aina hiyo unapaswa kwanza kuidhinishwa na mahakama.