1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU wapendekeza mazungumzo- uanachama wa Ukraine

8 Novemba 2023

Maafisa wakuu wa Umoja wa Ulaya wamependekeza leo hii kwamba Ukraine inapaswa kualikwa katika mazungumzo ya kujadili suala la uanachama wake katika Umoja huo ikiwa itakamilisha masharti ya mwisho.

https://p.dw.com/p/4YaMO
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: president.gov.ua

Leo hii, Tume ya Umoja huo ilikuwa ikitathmini iwapo Kyiv imepiga hatua katika mageuzi yake na kisha viongozi 27 wa Umoja wa Ulaya wataamua katika mkutano wa kilele mwezi Desemba iwapo mazungumzo hayo yanatakiwa kuanzishwa au la.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo hii kwamba  pendekezo la Tume ya Ulaya kufungua mazungumzo rasmi ya uanachama na Ukraine ni "hatua sahihi" kwa Kyiv na bara la Ulaya.

Soma pia:Urusi yaendelea kufanya mashambulizi katika eneo la Donetsk

Ukraine ilitangaza azma yake ya kuwa sehemu ya Umoja huo siku chache baada ya uvamizi wa Urusi na ilitangazwa rasmi kuwa mgombea wa kujiunga na EU mnamo mwezi Juni mwaka jana. Mataifa kama Uturuki, Albania, Montenegro, Macedonia Kaskazini na Serbia yamekwama kwa muda mrefu katika hatua hiyo ya mazungumzo.