1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Mawaziri wa mambo ya nje wa G7 wakutana Tokyo

7 Novemba 2023

Mawaziri wa mambo ya Nje wa Kundi la mataifa ya Magharibi yaliyoendelea kiviwanda G7, wanakutana Jumanne mjini Tokyo nchini Japan kujadili migogoro kati ya Israel na Hamas pamoja na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4YVeb
Annalena Baerbock / G7-Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani akiwa Tokyo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock akiwa Tokyo, JapanPicha: Sina Schuldt/picture alliance/dpa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili hii leo mjini Tokyo.

Viongozi wengine waliopo huko ni waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Analenna baerbock pamoja na ule wa Ufaransa Catherine Colonna ambaye amasema watajadili haja ya kujibu mahitaji ya raia huko Gaza na pia suala la kuheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu.

Mawaziri hao wa mahusiano ya kigeni wa G7 wanatarajia pia kujadili suala la mahusiano na Asia ya Kati yenye utajiri wa rasilimali, ushawishi wa China na kuandaa mazungumzo yajayo kati ya Rais Joe Biden wa Marekani na Xi Jinping wa China yanayotarajiwa huko San Francisco.