1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUANDA:Ndege za Angola kuharibiwa sifa

2 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmW

Nchi ya Angola huenda ikapiga marufuku ndege za mataifa ya Ulaya endapo Umoja wa Ulaya utaendelea na mpango wake wa kuharibu sifa ya kampuni yake ya ndege ya kitaifa.Umoja huo ulitangaza wiki jana kuwa unaongeza shirika la ndege la Angola ya TAAG katika orodha ya makampuni ya ndege yaliyohatari zaidi kusaifiria kote ulimwenguni.

Ndege za shirika hilo hazitaruhusiwa kusafiri hadi mataifa ya Umoja wa Ulaya kwasababu za kiusalama kwa mujibu wa Tume ya Umoja huo.Kulingana na Naibu Waziri wa Usafiri Helder Preza aliyezungumza na Radio ya kitaifa ya Angola…nchi yake huenda ikachukua hatua za kulipiza kisasi.Kampuni ya ndege ya kitaifa ya TAAG ya Angola inasafari za ndege hadi miji ya Paris,Ufaransa na Lisbon,Ureno.

Ndege za mashirika ya Air France,British Airways na TAP Air Portugal husafiri hadi mji mkuu wa Angola wa Luanda. Tangazo hilo la Umoja wa Ulaya lilitolewa Alhamsi iliyopita siku ambayo ndege ya kampuni ya TAAG aina ya Boeing 737 ilidondoka na kuanguka kwenye uwanja wa ndege kaskazini mwa Angola na kusababisha vifo vya watu watano.Serikali bado inafanya uchunguzi kujua chanzo cha ajali.