1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:UKIMWI NI SILAHA YA KUANGAMIZA UMMA

28 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFx0
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema katika mahojiano yaliotolewa leo hii kwamba UKIMWI umekuwa ni silaha ya maangamizi ya umma kwa baadhi ya nchi na kwamba dunia inaonekana kuwa inashindwa katika vita vyake dhidi ya janga hilo. Amewataka viongozi duniani kuchukuwa hatua zaidi za kuzuwiya kuenea kwa ugonjwa huo. Akizungumza na World Service radio ya Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC Annan amesema katika baadhi ya nchi wanazozingumzia UKIMWI ni silaha hasa ya maangamizi ya umma na kutaka kujuwa hatua gani wanayoichukuwa juu ya hali hiyo. Amesema hali hiyo inashiria aina fulani ya usugu usioaminika ambao usingeletegemewa kuwepo katika karne ya 21. Umoja wa Mataifa umesema katika repoti wiki hii kwamba vifo na kesi mpya za virusi vya HIV na UKIMWI vimefikia kiwango cha juu kisicho na kifani katika mwaka huu wa 2003 na inategemewa kuendelea kuongezeka. Takriban watu milioni 40 hivi sasa wanaishi na virusi vya HIV au na UKIMWI duniani kote.