1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Umoja wa Ulaya na Russia zaregezwa sheria za viza

5 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEUq

Umoja wa Ulaya na Russia zimeafikiana kuregeza sheria za viza.Makubaliano hayo mapya yatawarahisishia wanafunzi,wafanya biashara na wana diplomasia kusafiri kati ya Russia na nchi za Umoja wa Ulaya.Maafikiano hayo yalipatikana wakati wa mkutano uliofanywa kati ya rais Vladimir Putin wa Russia na waziri mkuu wa Uingereza,Tony Blair mjini London.Uingereza hivi sasa imeshika urais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka kila miezi sita.Mkutano wa London ulihudhuriwa pia na maafisa wengine wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya.Baadae waziri mkuu Blair aliwaambia maripota kuwa makubaliano yaliopatikana yatakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.Akaongezea kuwa aliitumia fursa ya mkutano huo kuyajadili masuala yanayosababisha wasi wasi katika Umoja wa Ulaya,kama vile hali ya haki za binadamu nchini Russia na pia mgogoro wa Chechnya.