1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Hispania yakiuka haki za binadamu yasema Amnesty Internatioanl.

9 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CETg

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu mjini London Amnesty International limesema kuwa maafisa wa serikali ya Hispania wanakwenda kinyume na mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu kwa kuwafukuza wahamiaji wa Kiafrika ambao wameingia katika eneo la Hispania nchini Morocco.

Shirika hilo linadai kuwa viongozi hao wamewafukuza wahamiaji hao kutoka mataifa yaliyoko kusini mwa jangwa la Sahara bila ya kujali hali yao kama wakimbizi wa kiuchumi ama watu wanaotafuta hifadhi ya kisiasa.

Katika kundi la kwanza ambalo limerejeshwa kutoka katika eneo la Melilla, watu 73 kutoka Mali walirejeshwa katika mji wa Tangiers nchini Morocco. Haijafahamika kile kilichowafika watu hao baada ya kuwasili katika bandari nchini Morocco.