1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lissu ataka polisi ya Tanzania iimpe ulinzi

Admin.WagnerD21 Julai 2020

Kiongozi wa upinzani wa Tanzania aliyenusurika kuuwawa kwa kupigwa risasa miaka mitatu iliyipita yupo katika maandalizi ya mwisho kurejea nyumbani Tanzania.

https://p.dw.com/p/3fea0
Tundu Lissu und Harrison Mwilima
Picha: DW/M. Fischer

Mwanasiasa machachari ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama kiku cha upinzani nchini Tanzania Chadema, Tundu Lissu amelitaka jeshi la polisi kumpatia ulinzi wakati ataporejea nchini humo Jumatatu ijayo. Lissu ambaye ametangaza kuwania urais kupitia chama chake katika uchaguzi wa Oktoba, amesema leo kuwa anakamilisha mipango ya kurejea nyumbani baada ya kuwa nje ya nchi kwa takribani miaka mitatu.

Lissu apanga kuwasili rasmi Tanzania Jumatano ya Ijayo.

Tundu Lissu Abgeordneter und Oppositionspolitiker überlebte ein Attentat in Tansania
Makamo mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu LissuPicha: DW

Mwanasiasa huyo anayeishi ughaibuni tangu aliponusurika jaribio la mauwaji Septemba 7, 2017 amesema amejipanga kurejea nyumbani na amedokoza kuwa anatarajia kukanyaga tena ardhini ya Tanzania Jumatatu ijayo mchana. Akizungumza na Watanzania kwa njia ya teknolojia ya video, Lissu aliyeonyesha nia ya kuwania urais kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake amesema anatambua jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda usalama wa raia hivyo anaamini wakati atakapowasili nchini suala hilo litazingatiwa katika kulinda maisha yake.

Kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 wa Tanzania

Lissu amesema anarejea nchini kushiriki mchakato wa uchaguzi mkuu na amewahimiza wananchi kutojiweka kando na uchaguzi huu.Lissu ni miongoni mwa makada saba wa chama hicho ambao wamerejesha fomu wakitaka ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao. Chama chake kimekuwa na vikao vya ndani kutathmini majina ya wagombea wote kabla ya majina hayo kujadiliwa na kamati kuu na baadaye mkutano mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwezi ambao ndiyo utaamua hatma ya jina lipi lipite.

Lissu anarejea nchini wakati vuguvugu la uchaguzi wenyewe likiwa juu na tayari karibu vyama vyote vinakamilisha pilikapilika za kuwapata wagombea wake. Je kurejea kwake nchini kunaweza kubadili upepo wa kisasa na hata usalama wa maisha yake utakuaje ? Ezekiel Kamwaga mbali ya kuwa mwandishi wa habari wa siku nyingi lakini pia amekuwa akifuatilia kwa karibu siasa za Tanzania.

Soma zaidi:Tundu Lissu atangaza nia ya kugombea urais Tanzania

Tume ya taifa ya uchaguzi imesema leo uchaguzi mkuu utafanyika siku ya Jumatato ya tarehe 28, mwezi Oktoba ikiwa ni tofauti na ilivyozoeleka katika chaguzi zilizopita zilizokuwa zikifanyika Siku ya Jumapili.