1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Libya yawarudisha wahamiaji wa Misri nchini mwao

Sylvia Mwehozi
1 Februari 2024

Mamlaka nchini Libya hapo jana zilianza kuwarudisha wahamiaji 350 kutoka Misri wasiokuwa na vibali, kupitia mamlaka iliyoundwa ya kupambana na uhamiaji kinyume cha sheria.

https://p.dw.com/p/4bvoa
Mgogo wa kiutu | Wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya
Watu wanaosadikiwa kuwa wahamiaji wakiwa katika mashua wakijaribu kuingia UlayaPicha: Jordan Pettitt/PA Wire/empics/picture alliance

Msemaji wa chombo hicho Kanali Haytham Belgassem Ammar ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mamlaka imeanza mchakato wa kuwarudisha raia 350 wa Misri walioko nchini humo bila vibali.

Mamlaka hiyo ilisema wahamiaji 323 raia wa Nigeriaambao wengi walikuwa wanawake, walirudishwa nchini mwao kutoka mji mkuu Tripoli na mji wa Kaskazini Magharibi Benghazi.

Soma pia:Mpango wa Sunak bado unakabiliwa na changamoto chungunzima

Mwaka jana, tawala hasimu za Libya zilikubaliana kuhusu chombo cha kupambana na uhamiaji kinyume cha sheria. 

Libya, taifa linalozongwa na machafuko limekuwa kama kivuko muhimu kwa wahamiaji wanapitia pwani ya Mediterania, kaskazini mwa Afrika, wakitokea sehemu nyingine za Afrika katika safari yao ya hatari wakilenga kufika Ulaya.