Watu zaidi ya 6,000 wapoteza maisha kujaribu kuingia Ulaya
9 Januari 2024Matangazo
Shirika la kutetea haki za wahamiaji nchini Uhipania limesema wahamiaji wasiopunguwa 6,618 walikufa au kutoweka wakijaribu kuingia Uhispania kupitia njia ya bahari mwaka 2023.
Idadi hiyo ni takriban mara tatu zaidi ya iliyorikodiwa katika mwaka uliotangulia 2022, ambapo wahamiaji 2,390 walipoteza maisha.
Jumla ya watoto 384 ni miongoni mwa wahanga kwa mujibu wa shirika hilo linalokusanya data kutoka kwa familia za wahamiaji waliokufa au kutoweka pamoja na takwimu zinazotolewa na maafisa wa shughuli za uokoaji.
Vifo vingi vya idadi ya wahamiaji iliyotajwa vimetokea katika bahari ya Atlantiki, ambayo inatumiwa kama njia ya kutoka Afrika kuingia visiwa vya Canary vya Uhispania.