1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya yasalimisha zana zake za uundaji wa silaha.

7 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFfI

WASHINGTON:
Libya imo njiani kusalimisha zana zake za
mwisho za uundaji wa silaha za kuangamiza.
Zaidi ya tani 500 za zana za silaha kutoka
Libya zimo njiani kupelekwa Marekani kwa meli,
aliarifu msemaji wa Rais wa Marekani George W.
Bush. Baada ya kufanyika mapatano yaliyodumu
miezi kadha kati yake na maafisa wa Kimarekani
na Kiingereza, hapo mwezi wa Disemba Libya
ilitangaza rasmi kuwa haina niya tena ya kuunda
silaha za kuangamiza. Uamuzi huo umechangia
kuikomboa Libya kutoka hali ya kutengwa
kimataifa.