1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya yasalimisha zana zake za uundaji wa silaha.

7 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFfF
WASHINGTON: Libya imo njiani kusalimisha zana zake za mwisho za uundaji wa silaha za kuangamiza. Zaidi ya tani 500 za zana za silaha kutoka Libya zimo njiani kupelekwa Marekani kwa meli, aliarifu msemaji wa Rais wa Marekani George W. Bush. Baada ya kufanyika mapatano yaliyodumu miezi kadha kati yake na maafisa wa Kimarekani na Kiingereza, hapo mwezi wa Disemba Libya ilitangaza rasmi kuwa haina niya tena ya kuunda silaha za kuangamiza. Uamuzi huo umechangia kuikomboa Libya kutoka hali ya kutengwa kimataifa.