1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Libya yafikia makubaliano ya mafuta na gesi na Italia

26 Januari 2023

Shirika la Mafuta la taifa nchini Libya, NOC, limearifu kufikia makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 8 na kampuni kubwa ya mafuta ya Italia ya ENI.

https://p.dw.com/p/4MjaS
Libyen | Öl- und Gas Bohrinsel im Mittelmeer
Picha: Antonio Sempere/Europa Press/abaca/picture alliance

Mkuu wa NOC Farhat Bengdara amekiambia kituo cha habari cha nchini humo cha Al-Masar kwamba wamefikia makubaliano hayo ya kuendeleza sekta ya gesi na mafuta kwa kuyaendeleza maeneo mawili yaliyopo kwenye pwani yake na yatakayokuwa na uwezo wa kuzalisha futi za ujazo milioni 850 za gesi kwa siku.

Hata hivyo kampuni ya ENI haikuwa tayari kuzungumza chochote juu ya makubaliano hayo yanayotarajiwa kusainiwa rasmi siku ya Jumamosi.

Italia imekuwa ikihangaika kusaka mbadala wa nishati ya Urusi tangu taifa hilo lilipoivamia Ukraine na waziri mkuu Giorgia Meloni anatarajiwa kuzuru Tripoli siku zijazo, hii ikiwa ni kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya mataifa hayo mawili.