1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya kuteketeza silaha zake za kuangamiza.

20 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFqk
TRIPLOS: Baada ya kufanyika mapatano ya kisiri yaliyodumu miezi tisa Libya imetangaza inataka kuteketeza silaha zake zote za kuangamiza na kufunga miradi yake yote ya kuunda silaha kama hizi. Pia wakaguzi wa silaha wa kimataifa wataweza kuingia Libya wakati wowote ule. Rais Muammar el Ghaddafi alisisitiza kuwa Libya imefikia uamuzi huo ili kuzitia moyo nchi nyingine zichukue zifuate mfano wake. Maridhio hayo ya Rais Ghaddafi yamekaribishwa kimataifa. Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Jack Straw alipongeza zile ishara zilizotolewa na Iran za kuwafungulia milango wakaguzi wa silaha wa kimataifa. Zikituwama ripoti zao juu ya habari za maafisa wa serikali zao, vyombo vya habari vya Kimarekani na Kiingereza viliarifu kuwa Libya ilikuwa njiani kuunda silaha za kinyuklea, ikiwa tayari inadhibiti silaha za kemikali, na kuwa na uwezo wa kuunda silaha za kibiolojia. Lakini kwa kulingana na habari za mashirika ya upelelezi, matawi mbali mbali ya uundaji silaha za kuangamiza ya Libya hayakuendelezwa zaidi ya daraja ya utafiti.