1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LIBYA KUJITENGA NA SILAHA ZA MAANGAMIZI

20 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFqu
LONDON: Libya imekubali kuachilia mbali miradi yake inayohusika na silaha za maangamizi.Hayo walitangaza waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair na Rais George W.Bush wa Marekani.Katika hotuba za ghafla walizotoa kwenye televisheni mijini London na Washington takriban wakati mmoja,Blair na Bush walieleza kuwa Uingereza na Marekani zilikuwa zikijadiliana na Tripoli tangu miezi 9 ya nyuma kuhusu silaha zilizopigwa marufuku.Blair akaongezea kuwa uamuzi wa Libya kuachilia mbali mipango yake ya kutengeneza silaha za maangamizi,huipa nchi hiyo haki ya kurejea katika kile alichokiita"jumuiya ya kimataifa".Uingereza ikaendelea kusema kwamba Libya ilikaribia kutengeneza bomu la kinyuklia na ilikuwa ikishirikiana na Korea ya Kaskazini,kurekebisha makombora ya Scud,kabla ya kukubali kuachilia mbali mpango wake wa kutengeneza silaha za maangamizi.Rais Bush wa Marekani kwa upande wake amesema Libya itaweza kuwa na uhusiano bora zaidi na Marekani ikiwa kweli itatekeleza ahadi ya kuachilia mbali miradi ya silaha za maangamizi.