1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya ilikiuka Mkataba wa Kueneza Silaha za Kinyuklea.

21 Februari 2004
https://p.dw.com/p/CFgV

VIENNA: Kwa mujibu wa uchunguzi wa Shirikia la Kimataifa la Kinyuklea, Libya imekiuka ule Mkataba wa Kimataifa wa Kukataza Usambazaji wa Silaha za Kinyuklea. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika hilo la UM, Libya ilikuwa na uwezo wa kutengeneza madini ya Plutonium kwa shabaha ya kuunda silaha za kinyuklea. - Hapo mwezi wa Disemba, kiongozi wa Libya Muammar al Ghaddafi alitangaza kuwa nchi yake inasitisha miradi yake yote ya kuunda silaha za kuangamiza na kuwafunguliwa milango wakaguzi wa kimataifa wa silaha kufanya ukaguzi wao nchini Libya. Hapo wiki ijayo, mkuu wa Shirika hilo la Kimataifa la Kinyuklea, Mohammed al Baradei anataka kwenda tena mji mkuu wa Libya, Tripolis kuchunguza maendeleo yanayofanywa na wakaguzi wake wa silaha.