1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lebanon: mwaka mmoja tangu mlipuko katika bandari ya Beirut

Zainab Aziz Mhariri: Gakuba, Daniel
4 Agosti 2021

Watu wa Lebanon wanakumbuka maafa yaliyosababishwa na mlipuko kwenye bandari ya Beirut mwaka mmoja uliopita, huku biashara na mabenki yakiwa yamesambaratika. Watu zaidi ya 200 walikufa kutokana na ajali hiyo.

https://p.dw.com/p/3yWM9
Beirut Libanon Hafen Explosion Statue
Picha: JOSEPH EID/AFP via Getty Images

Muda mfupi baada ya saa 12 jioni mnamo Agosti tarehe 4, mwaka jana mlipuko mkubwa ulitikisa mji wa Beirut uliotokea kwenye ghala moja katika bandari ya mjini humo hali iliyoifanya Lebanon kuonekana kama eneo la vita. Wakati Walebanon wanayakumbuka maafa hayo, nchi yao inapitia kipindi cha mgogoro wa kiuchumi na wa mabenki kisichokuwa na kifani katika historia ya nchi yao.

Soma zaidi:Unatimia mwaka mmoja tangu mripuko mkubwa wa Beirut

Pamoja na hayo Lebanon inakabiliwa na mkwamo wa kisiasa uliosababisha nchi hiyo kutokuwa na serikali imara kwa muda wa mwaka mzima sasa. Khose Khilichian ni mkazi wa eneo la Bourj Hammoud kitongoji kimojawapo karibu na bandari ya Beirut amesema tukio hili halitasahaulika maisha.

Lebanon: Pichani sanamu lililotengenezwa na mtalaam wa ujenzi Nadim Karam kuadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea mlipuko kwenye badanari ya Beirut tarehe 04.08.2020.
Lebanon: Pichani sanamu lililotengenezwa na mtalaam wa ujenzi Nadim Karam kuadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea mlipuko kwenye badanari ya Beirut tarehe 04.08.2020.Picha: MOHAMED AZAKIR/REUTERS

Familia za watu waliokumbwa na athari za mlipuko zimepanga kufanya maombolezo kwenye sehemu ya bandari iliyoteketezwa kutokana na mlipuko. Watu pia walipanga kufanya maandamano makubwa. Miito ya kutaka haki itendeke ilitolewa na baadhi ya washiriki, ambao wameilamu serikali kwa kusema kwamba ndiyo iliyohusika na maafa yaliyotokea. Hata hivyo mpaka sasa hakuna aliewajibishwa kwa mlipuko huo.

Ulaya huenda ikwawekea vikwazo wanasiasa wa Lebanon

Watu zaidi ya 200 walikufa wa wengine maalfu walijeruhiwa. Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema Umoja wa Ulaya unaweza kuwawekea vikwazo wanasiasa wa Lebanon ikiwa hawatafanya juhudi za kuunda serikali na kupitisha hatua za kuleta mageuzi muhimu ya kiuchumi.

Waziri wa Mamno ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas
Waziri wa Mamno ya Nje wa Ujerumani Heiko MaasPicha: Xander Heinl/photothek/picture alliance

Waziri Maas amesisitiza kwamba ni sahihi kwa Umoja wa Ulaya kuendeleza shinikizo dhidi ya viongozi wanaofanya maamuzi nchini Lebanon. Hata hivyo waziri Maas amehakikisha kwamba Ujeruamni itaendelea kuziunga mkono asasi za kiraia na ameahidi msaada zaidi kwa watu wa Lebanon.

Tazama:

Tahadhari kuhusu mdororo wa kiuchumi Lebanon

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ameeleza kuwa Ujerumani inashika nafasi ya pili miongoni mwa wafadhili wanaoisaidia Lebanon katika msingi wa uhusiano wa pande mbili. Aidha, Maas amesikitika kwamba mpaka sasa hakuna hatua iliyopigwa katika kuunda serikali nchini Lebanon. Juhudi za kuunda serikali zilizofanywa na waziri mkuu mteule Saad Hariri zilishindikana mwezi uliopita baada ya miezi tisa ya mkwamo.

Vyanzo:/AP/RTRE/ https://p.dw.com/p/3yVUl