1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwa harakati za kijeshi kugharimia uundaji silaha

24 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhV
WASHINGTON: Rais wa Marekani George W. Bush ameilitaka bunge la Marekani liridhie pesa zaidi kwa matumizi ya kijeshi. Wizara ya Mambo ya Ulinzi iliarifu kuwa tathmini ya gharama za ulinzi katika bajeti ijayo inatazamia mwongezeka wa asili miya saba wa matumizi ya kijeshi yatakayofikia Dollar biliyoni 402. Waziri wa Mambo ya Ulinzi Donald Rumsfeld alisema, tathmini hiyo ya bajeti ya ulinzi ni ishara ya kujitolea kwa Rais Bush katika mapigano dhidi ya ugaidi. Kiwango hicho kilichotajwa hakiingizi gharama za matumizi ya kijeshi nchini Iraq na Afghanistan. Hivi sasa Marekani inatumia Dollar biliyoni kwa wiki kugharimia harakati za kijeshi nchini Iraq. Nchini Afghanistan Marekani hutumia Dollar biliyoni moja kwa mwezi kwa harakati za wanajeshi wake.