KUWAIT CITY: Washukiwa ugaidi wapewe adhabu ya kifo
12 Juni 2005Matangazo
Muendesha mashtaka wa serikali nchini Kuwait ametoa wito wa kutolewa adhabu ya kifo kwa watu 34 wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Qaeda.Sababu ya kutaka adhabu hiyo amesema ni kuwa wanamgambo hao wamefanya vitendo vya kigaidi,wamewauwa polisi kadhaa na pia walipanga kuwashambulia wanajeshi wa Marekani walio nchini Kuwait.Watuhumiwa hao wameyapinga mashtaka yote na wamesema kuwa waliteswa na polisi ili wapate kukubali mashtaka ya uongo.