1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KURA YA MAONI JUMAPILI UFARANSA:

27 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CHgn

Wapiga kura nchini Ufaransa wataamua kesho hatima ya katiba ya Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni ama kuikubali au kuikataa.Isipokuwa badiliko la nia la dakika ya mwisho,rais Jacques Chirac wa Ufaransa, anaelekea atashindwa kuwashawishi wafaransa kuidhinisha katiba hiyo.Ili kuwapa moyo wafaransa kuitikia “ndio” Bunge la pili la Ujerumani (Bundesrat) liliidhinisha jana kwa sauti kubwa katiba hiyo.

Rais wa zamani wa Ufaransa-alietunga katiba yenyewe Valery Giscard d’Estaing alikuwapo Bungeni Ujerumani wakati wa ikiidhinishwa.Isitoshe,jana mawaziri wawili wakuu-Kanzela Gerhard Schröder wa Ujerumani na Spain Rodriguez Zapatero wa Spain, wamekwenda Ufaransa katika jaribio lao la mwisho kuwashawishi wafaransa kuidhinisha katiba ya UU kabla ya kura ya kesho ya maoni.

Maoni ya wafaransa yakionesha kambi ya wanaoikataa katiba hiyo inaongoza siku 1 kabla ya kura viongozi wawili wa nchi jirani za Ulaya-Ujerumani na Ufaransa wanawalenga wafuasi wa chama cha kijamaa wanaoungamkono UU kubadili maoni yao na waipigie kura.Viongozi wa UU wameingiwa na homa ya wasi wasi kwamba kukataliwa kwa mkataba huo kesho na wapigakura wa Ufaransa kutakua pigo kubwa kwa katiba ya kwanza muhimu ya Umoja huo.Katiba yenyewe ina shabaha ya kurahisisha kanuni za kuendesha Umoja wenyewe.

Baada ya Ujerumani jana kuwa nchi ya 9 mwanachama kati ya zote 25 kuidhinisha katiba hiyo,Kanzela Schröder amepangwa kuhutubia mutano wa hadhara wa wale wanaoungamkono katiba mjini Toulouse,kusini mwa Ufaransa akiwa pamoja na waziri wa zamani wa Ufaransa Dominique Strass-Kahn.

Waziri mkuu wa Spain Zapatero –pia msoshalist kama Schröder, alipangwa kujiunga na kiongozi wa chama cha kisoshalist cha Ufaransa Francois Hollande katika mutano mwengine wa hadhara mjini Lille.Waziri mkuu wa Spian anarejesha hapo shukurani zake alizopewa na rais jacques Chirac wa Ufaransa aliezuru Spian kuungamkono kampeni hiyo ilipopigiwa kura katiba hiyo.Spain ilikua nchi ya kwanza ya UU kuipigia kura katiba na kuipitisha.

Kwa kuidhinisha jana Ujerumani, imefuata nyayo za Austria,Ugiriki,Hungary,Itali,Lithuania,Slovakia,Slöovenia na Spain.

Wanachama wote 25 wa UU wanapaswa kuidhinisha katiba hiyo ili iweze kuanza kazi.Endapo wapigakura nchini Ufaransa wakiitia munda hapo kesho na kuiangusha, basi UU utatumbukia mashakani,kwani Ufaransa ndiyo mojawapo ya dola 6 zilizuasisi Umoja wa Ulaya.

Ziara ya Schröder nchini Ufaransa wakati huu imekuja katika kipindi kigumu kwake kisiasa.Kwani ni punde baada ya kuitisha uchaguzi na mapema kufuatia kushindwa vibaya kwa chama chake katika mkoa huu wa Mto Rhein.

Tangu kanzela Schröder hata yule wa zamani Helmut Schmidt wametoa mwito wa dharura kwa wapigakura wa Ufaransa kuipigia kura kesho katiba hiyo.Alisema,

“Ulaya ina nguvu inapozungumza kwa sauti moja.Tunahitaji Ulaya yenye nguvu na ilioungana.”mwisho wa kumnukulu.

Katika hotuba yake kwa taifa juzi usiku katika hali ya kufadhahika, rais Jacques Chirac alitoa mwito wake wa mwisho kwa wafaransa kuiungamkono katiba ya UU katika kura ya kesho.

Gameti la mjini Paris Le Parisien lilijitokeza na kichwa hiki cha labari jana siku ya pili yake: “Wasi wasi mkubwa katika Qasri la rais la Elysee”.

Lakini licha ya mwito huo wa mwisho wa rais Chirac kwa wapiga kura ,uchunguzi wa maoni ungali ukionesha 55% ya wafaransa wanaipinga na 45% wanaoungamkono.Si ajabu macho yote ya walimwengu yanakodolewa Paris hapo kesho-kwani hukumu ya wafaransa bila shaka itaathiri hatima ya katiba hii kupitishwa na wanachama waliobakia pamoja nao Uingereza.