1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la G7 lasifu kuachiwa huru kwa mateka wa Israel

29 Novemba 2023

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya kundi la G7 wameikaribisha hatua ya kuachiwa huru mateka kadhaa waliochukuliwa na kundi la Hamas wakati wa shambulizi la Oktoba 7 ndani ya ardhi ya Israel.

https://p.dw.com/p/4ZYdQ
Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Kundi la G7 pamoja na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya.
Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Kundi la G7 pamoja na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya. Picha: Jonathan Ernst/Pool/dpa/picture alliance

Kupitia taarifa ya pamoja iliyotolewa usiku wa kuamkia leo wanadiplomasia hao wakuu wa G7 pia wametoa mwito wa kuachiwa mateka wote waliosalia haraka iwezekanavyo na bila ya masharti yoyote.

Vilevile wamesisitiza kuunga kwao mkono haki ya Israel kujilinda lakini wamesema hilo linapaswa kufanyika chini ya misingi ya sheria ya kimataifa na kuzingatia umuhimu wa kuwalinda raia.

Mawaziri hao kutoka mataifa ya Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Canada, Italia, Uingereza na Japan wamesema pia wanazikubali juhudi zote zinazofanywa kuwezesha urefushaji mkataba wa kusitisha mapigano kati ya Israel na Kundi la Hamas.

Kadhalika wameelezea kwamba wanapendelea suluhusho la kuundwa madola mawili huku wakitoa hadhari dhidi ya kutanuka kwa kwa mzozo wa sasa wa Mashariki ya Kati.