1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuna makundi 266 yanayomiliki silaha mashariki ya Kongo

Mitima Delachance19 Aprili 2023

Mpango wa kupokonya silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo unaofahamika kama PDDRCS, unatangaza kwamba umehesabu jumla ya makundi yenye silaha 266 katika majimbo matano ya mashariki ya Kongo

https://p.dw.com/p/4QHn6
DR Kongo Rethy | militante Milizgruppe URDPC/CODECO
Picha: ALEXIS HUGUET/AFP

Mpango huo umeyaonya makundi hayo na kuyataka kuweka chini silaha. Kutoka Bukavu. Kati ya makundi hayo yenye silaha yako makundi mia mbili hamsini na mbili yanayoundwa na raia wa Kongo na makundi mengi 14 yenye silaha ambayo ni ya kigeni.

 Zaidi ya watu 40 wauawa katika mashambulizi DRC

Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki linaendesha operesheni Kongo
Kikosi cha kikanda kipo mashariki mwa KongoPicha: Alexis Huguet/AFP

Wakati wa mkutano na waandishi habari siku ya Jumanne, mratibu wa mpango wa kuwapokonya silaha wapiganaji wa zamani na kuwarejesha tena katika maisha ya kawaida Tomy Tambwe alisema kuwa takwimu hizi zilipatikana baada ya hesabu iliyofanywa katika majimbo matano ya mashariki mwa DRC. Majimbo hayo ni Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Maniema na Tanganyika. Mratibu wa mpango wa upokonyaji silaha Tomy Tambwe anaeleza zaidi.

"Kwa mujibu wa nyaraka zetu, jimbo la Ituri lina makundi ishirini yenye silaha, Kivu Kaskazini ina makundi sitini na nne yenye silaha, Kivu Kusini ina makundi yenye silaha mia moja thelathini na sita, Maniema ina makundi ishirini yenye silaha na Tanganyika kumi na tisa. Pia kuna vikundi vya nje vyenye silaha lakini kwetu sisi kazi ambayo tuliombwa ni kubaini makundi haya yenye silaha na kujua chanzo cha vikundi hivyo kumiliki silaha. Na hii ilituongoza kuchora ramani ya makundi yenye silaha jimbo kwa jimbo na wilaya kwa wilaya”.

Tomy Tambwe anawaomba Wakongo wote, ambao wamechukua silaha, kujiondoa kwa kufuata wito wa Rais wa Kongo Félix Antoine Tshisekedi wa kutaka amani irejee nchini kote, akisema harakati hii ya mpango wa PDDRCS ilikuwa pia fursa ya kubaini chanzo cha migogoro katika majimbo hayo. Kwa mara nyingine anaeleza:

"Tumebaini migogoro minane inayojitokeza mara kwa mara katika majimbo haya. Kuna migogoro ya mipaka, migogoro kati ya hifadhi za taifa na vijiji, migogoro ya urithi wa mamlaka ya kimila, kuna migogoro ya ardhi, migogoro ya madini, migogoro ya kiutawala, migogoro ya mazingira na migogoro ya kikabila”.

Hata hivyo, baadhi ya wadadisi wa mambo wanahisi kwamba mpango huu umechelewa na haujaendelea kulingana na matarajio ya raia wa Kongo. Augustin Ntayitunda mchambuzi wa masuala ya kiusalama, anapendekeza kwamba serikali ya Kongo ijihusishe zaidi na makundi ya silaha kutoka nchi za kigeni yanayopora mali za Kongo:

Wakati wa ziara yake Kivu Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais wa Uswizi Alain Berset alionya kuundwa kwa hali ya amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mitima Delachance, DW, Bukavu.