1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Kuleba apigia debe uanachama wa Ukraine Umoja wa Ulaya

11 Desemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amezitolea mwito nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuunga mkono hatua ya kuanzisha mazungumzo na nchi yake kuhusu dhamira yake ya kutaka kuwa mwanachama.

https://p.dw.com/p/4a223

Kuleba amesema ikiwa Umoja huo utaamuwa kutounga mkono kuanzishwa mazungumzo hayo baadae wiki hii,hatua hiyo itakuwa na athari mbaya na itawavunja moyo watu wa Ukraine.

Kuleba ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akiwasili Brussels ambako atakutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya.

Amesisitiza kwamba Kiev iko kwenye mkondo wa kutimiza vigezo vinavyohitajika kujiunga na jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kupambana na rushwa na kuimarisha haki za makundi ya walio wachache.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanahitajika kuamuwa kwa pamoja kuhusu Ukraine ingawa tayari waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban mara kadhaa amesema haungi mkono kaunzishwa mazungumzo hayo.