1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kusini yathibitisha kurejesha mahusiano na Japan

21 Machi 2023

Korea Kusini imethibitisha leo kwamba imerudisha mahusiano mazuri ya kijeshi yanayohusisha ubadilishanaji taarifa za kijasusi na Japan.

https://p.dw.com/p/4OyP1
Japan | Yoon Suk Yeol und Fumio Kishida
Picha: Kyodo/IMAGO

Hayo ni wakati nchi hizo mbili zikiimarisha mahusiano yao kufuatia kuongezeka vitisho kutoka Korea Kaskazini.

Hatua hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini imefuatia mkutano wa kilele kati ya viongozi wa nchi hizo, rais Yoon Suuk Yeol wa Korea Kusini na waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida mjini Tokyo wiki iliyopita.

Soma pia: Japan na Korea Kusini zatangaza hatua za kurejesha uhusiano

Kupitia mazungumzo hayo yaliyofanyika baada ya miaka 12, nchi hizo zilikubaliana kurudisha mahusiano mazuri yaliyoharibiwa na mivutano ya kihistoria iliyotokana na utawala wa miaka 35 wa kikoloni wa Japan katika rasi ya Korea.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW