1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan na Korea Kusini zatangaza hatua za kurejesha uhusiano

16 Machi 2023

Japan na Korea Kusini zimetangaza hatua ya kulegeza vizingiti vya biashara baina yao na kurejea kwenye utaratibu wa kuwawezesha viongozi wa nchi hizo kutembeleana mara kwa mara.

https://p.dw.com/p/4OmbR
Südkoreas Präsident Yoon Suk Yeol und Japans Premierminister Fumio Kishida
Picha: Ahn Jung-won/Yonhap/AP/picture alliance

Hayo yametokana na ziara ambayo Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol anaifanya nchini Japan. Kwa muda wa miaka mingi nchi hizo jirani zimekuwa na uhasama kutokana na kutumikishwa kwa nguvu kwa Wakorea wakati wa vita.

Tangu kuchaguliwa mwaka jana Yoon alieleza wazi kwamba jambo la kipaumbele katika sera zake ni kuujenga upya uhusiano mzuri na Japan.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Japan Yumio Kishida, amesema nchi yake na Korea Kusini zimekubaliana kuanzisha tena michakato ya kidiplomasia.

Michakato hiyo ni pamoja na uwezekano wa Kishida kumwalika Yoon kuhudhuria mkutano wa nchi saba tajiri duniani, G7 utakaofanyika mjini Hiroshima mnamo mwezi Mei.