1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yashindwa kurusha satelaiti

31 Mei 2023

Jaribio la Korea Kaskazini la kurusha satelaiti yake ya kwanza ya kijasusi halikufanikiwa baada ya roketi hiyo "kuanguka baharini."

https://p.dw.com/p/4S0CC
Kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong Un, akiwa na bintiye na maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi, 20.03.2023, wakitazama mazoezi ya kijeshi katika eneo ambalo halikutajwa, hii ikiwa ni kulingana na KNCA ya Korea Kusini.
Jamii ya kimataifa ina wasiwasi na mipango ya makombora ya Korea kaskazini, ikisema inahatarisha usalama wa kikanda. Picha: KCNA/KNS/dpa/picture alliance

Shirika la habari la serikali limeripoti kuwa, urushaji wa satelaiti hiyo ulifanyika leo, katika siku ya kwanza kati ya siku 12 za majaribio ya kuirusha roketi hiyo katika mzingo wa dunia. Korea Kaskazini haina satelaiti inayofanya kazi angani na kiongozi wake Kim Jong Un ametilia mkazo uundaji wa satelaiti ya kijasusi kuwa moja kati ya kipaumbele cha utawala wake. Mamlaka Pyongyang imesema itachunguza changamoto za kiufundi zilizojitokeza katika urushaji wa satelaiti hiyo na kuchukua hatua za haraka kuzirekebisha na kuirusha tena haraka iwezekanavyo. Jeshi la Korea Kusini liligundua kurushwa kwa satelaiti hiyo na kusema kwamba ilipotea kwenye rada na kuanguka kwenye bahari. Jana Jumanne, Korea Kaskazini iliweka wazi mpango wake wa kurusha kile ilichokiita satelaiti ya anga ya upelelezi kabla ya Juni 11 na tayari ilikuwa imeielezea Japan juu ya mpango wake huo.

Soma Zaidi: Japan itaharibu kombora litakalorushwa na Korea Kaskazini