1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yarusha makombora mawili bahari ya mashariki

31 Agosti 2023

Korea Kaskazini imesema imerusha makombora mawili ya masafa mafupi kama sehemu ya "mazoezi ya kimbinu ya nyuklia" yaliyochochewa na luteka za kijeshi za Marekani na Korea Kusini.

https://p.dw.com/p/4VmGD
Korea Kaskazini imefanya majirio kadhaa ya makombora
Korea Kaskazini imefanya majirio kadhaa ya makomboraPicha: YNA/picture alliance

Jeshi la Korea Kaskazini limesema katika taarifa kuwa, makombora hayo yalirushwa jana jioni katika kile kilichoelezwa kuwa ni "mazoezi ya kimkakati ya shambulio la nyuklia."

Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap, likinukuu jeshi la nchi hiyo kuwa, makombora hayo yalirushwa kuelekea bahari ya mashariki ambayo pia inafahamika kama bahari ya Japan.

Urushaji huo wa makombora - ulioripotiwa kwa mara ya kwanza na jeshi la Korea Kusini - umetokea katikati ya luteka za kijeshi za kila mwaka zinazofanywa na Marekani na Korea Kusini, na aghalabu kuikasirisha Pyongyang.

Jeshi la Korea Kaskazini limesema katika taarifa kuwa, urushaji wa makombora hayo unalenga kutuma ujumbe kwa maadui.

Pyongyang imefanya majaribio kadhaa ya makombora mwaka huu.