1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kusini

Marekani yapeleka ndege zaidi za kivita Korea Kusini

30 Agosti 2023

Ndege za kivita chapa B-1B za marekani zimepelekwa kwa ajili ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Korea Kusini na Japan.

https://p.dw.com/p/4VkNT
Südkorea KAI T-50 Kampfjet
Picha: LAT Photographic/IMAGO

Kulingana na wizara ya ulinzi ya Korea Kusini, ndege hizo zimeruka kwa pamoja na ndege za FA-50 za Korea Kusini kama sehemu ya luteka hizo za kijeshi. Ndege hizo pia ziliungana na zengine 12 za kivita kutoka Japan.

Marekani imetuma ndege hizi zilizo na uwezo wa kurusha mabomu siku chache baada ya Korea kaskazini kujaribu kurusha setlaiti, zoezi lililotibuka. Marekani na Korea Kusiniwalianza mazoezi hayo ya kijeshi waliyoyapa jina Ngao ya Uhuru ya Ulchi wiki iliyopita.

Lengo la mazoezi hayo ni kuzidisha jawabu lao kwa kitisho cha Korea Kaskazini kinachoongezeka cha makombora ya nyuklia. Sehemu ya pili ya mazoezi hayo yataanza Jumatatu ijayo.