1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yaandikisha wapiga kura

17 Februari 2023

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, CENI, inaendelea na zoezi la uandikishwaji wa wapiga kura katika majimbo ya mashariki, licha ya majimbo hayo kukabiliwa na changamoto za kiusalama.

https://p.dw.com/p/4Nf0C
Niger | Präsidentschaftswahlen in Zinder
Picha: Mohamed Tidjani Hassane/DW

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, CENI, inaendelea na zoezi lililoanzishwa jana la kuwaandikisha wapiga kura katika majimbo ya mashariki, licha ya majimbo hayo kukabiliwa na changamoto za kiusalama. Raia katika mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini -Goma walipanga msururu kwa muda mrefu ili kujisajili kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba.

Gavana wa kijeshi wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Luteni Jenerali Constantin Ndima aliwaeleza waandishi wa habari kwamba maafisa wa jeshi na wa polisi wamesambazwa ili kuhakikisha usalama wakati wa mchakato huo. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  ina historia ndefu ya misukosuko ya kisiasa na chaguzi zenye utata.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2018, kwa mara ya kwanza taifa hilo lilishuhudia ubadilishanaji wa madaraka ya urais kwa njia ya amani, na kuchaguliwa kwa kiongozi wa zamani wa upinzani Felix Tshisekedi, ingawa matokeo yalipingwa vikali na wapinzani wake.