1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la dunia la wanawake laendelea kutimua vumbi

Sylvia Mwehozi
23 Julai 2023

Michuano ya Kombe la dunia kwa Wanawake inaendelea huko New Zealand na Australia. Sweden imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kusini katika mechi iliyochezwa Jumapili.

https://p.dw.com/p/4UHYK
Kombe la Dunia la wanawake 2023 | England v Haiti
Wachezaji wa England na Haiti wakichuana Picha: DAN PELED/REUTERS

Michuano ya Kombe la dunia kwa Wanawake inaendelea huko New Zealand na Australia. Sweden imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kusini katika mechi iliyochezwa leo.

Marekani ilianza vyema kampeni yake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Vietnam. Marekani iliyo katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa FIFA inatafuta kushinda taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Wawakilishi wengine wa Afrika timu ya Zambia, ilichapwa mabao 5-kwa 0 na timu ya Japan. England waliwalaza Haiti bao 1-0 kwa nunge. Denmark ilihitimisha dakika 90 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya China.

Uholanzi imepata alama tatu mbele ya Ureno katika mchezo uliomalizika kwa bao 1-0 Ufaransa wanavaana na Jamaica mchana wa Jumapili.