1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoZambia

Zambia yagaragazwa 5-0 na Japan

22 Julai 2023

Timu ya kina dada ya Marekani imeanzisha juhudi zake ya kunyakua taji la tatu mfululizo la Kombe la Dunia la Wanawake kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Vietnam usiku ya kuamkia leo.

https://p.dw.com/p/4UGAk
OCEAUNZ Spielball FIFA Fußball Frauen-WM Australien und Neuseeland
Picha: Kolvenbach/IMAGO

Mshambuliaji wa Marekani Sophia Smith aling'ara katika ngarambe hii ndani ya uwanja wa Eden Park huko Auckland, akifunga mara mbili na huku nahodha Lindsey Horan akipachika wavuni bao la tatu na la ushindi katika mechi iliyotazamwa na zaidi ya mashabiki 41,000.

Katika mechi nyengine mabingwa wa mwaka 2011 Japan wameicharaza Zambia mabao 5-0 katika uga wa Waikato mapema leo.

Soma pia: Kombe la Dunia: Zambia itamkosa Chanda dimbani

Mchezaji Hinata Miyazawa alicheka na wavu mara mbili huku Mina Tanaka na Jun Endo wakiongeza bao moja moja. Kunano dakika ya za lala salama mlinda lango wa Zambia Catherina Musonda alionyeshwa kadi nyekundi na kuipa Japan penati ambayo bao la tano lilitiwa kimyani na mchezaji Riko Ueki.

Zambia inakabiliwa na mapambano magumu ili kufuzu kwa hatua ya 16 bora kwa mechi dhidi ya Uhispania na Costa Rica kama wapinzani wake wanaofuata.