1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kologne.Maonyesho ya zana za upigaji picha yafunguliwa mjini Kologne.

26 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD8l

Maonyesho makubwa ya kibiashara ya zana za upigaji picha kwa jina la fotokina yamefunguliwa hii leo katika jiji la Kolon nchini Ujerumani.

Maonyesho hayo yanayofanyika kila baada ya miaka miwili yanaendelea kumurika maendeleo ya kiteknolojia yaliyopatikana kuanzia upigaji picha asilia kufikia utaratibu wa kisasa wa digital.

Katika wakati ambapo bei zinatarajiwa kupungua, wanaviwanda vya picha wanatarajia, wapiga picha wasio wa kulipwa kuwavutia na kuwekeza katika kamera za kisasa za Digital.