1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kitisho cha bomu chafunga shule Ufaransa

16 Oktoba 2023

Wanafunzi katika shule moja ya wilaya ya Arras kaskazini mwa Ufaransa wameondolewa kwa tahadhari kufuatia taarifa ya kuwepo kwa bomu.

https://p.dw.com/p/4Xa5r
Messerattacke Frankreich Schule
Wazazi katika skuli ya Arras baada ya mwalimu mmoja kuuawa kwa kuchomwa kisu.Picha: Pascal Rossignol/REUTERS

Hayo yametokea katika shule ambayo mwalimu mmoja aliuawa kwa kuchomwa kisu wiki iliyopita katika shambulizi linaloaminika kuwa lilitendwa na wafuasi wa itikadi kali za kidini.

Mamia ya wafanyakazi na wanafunzi wameondoka katika shule hiyo, huku Rais Emmanuel Macron akikatiza mipango ya safari zake nje ya nchi siku ya Jumatatu (Oktoba 15) ili kuandaa mkutano wa usalama.

Soma zaidi: Polisi wafanya msako baada ya kitisho cha bomu Ufaransa

Mamlaka ya mkoa wa Pas-de-Calais imesema kuwa hatua zote za tahadhari na kiusalama zimechukuliwa.

Kufuatia tukio hilo la mwalimu kuchomwa kisu, Ufaransa iko katika hali ya tahadhari dhidi ya vitisho vinavyohofiwa kupangwa na magaidi.