1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wafanya msako baada ya kitisho cha bomu Ufaransa

14 Oktoba 2023

Watu waliokuwa katika makumbusho ya Louvre mjini Paris na Kasri la mji wa Versailles la nchini Ufaransa wamelazimika kuondoka kwenye majengo hayo.

https://p.dw.com/p/4XXXA
Paris Louvre Museum geräumt | Terrorwarnung
Picha: SARAH MEYSSONNIER/REUTERS

Polisi mjini Paris wamesema kuwa maafisa wake wamefanya  msako katika Makumbusho ya Louvre mara  baada ya kupokea kitisho hicho. Idara ya mawasiliano ya makumbusho hayo imesema hakuna mtu aliyejeruhiwa wala tukio lolote baya lililotokana na kitisho hicho.

Soma pia: Macron aagiza usalama kuimarishwa Ufaransa

Serikali ya Ufaransa imekuwa katika tahadhari kubwa baada ya mwalimu mmoja kuchomwa kisu katika mji wa mji wa Arras jana Ijumaa. Mapema leo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, aliagiza kuongezwa kwa wanajeshi 7,000 ili kuimarisha usalama nchini humo