1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa wabunge wa siasa kali Ujerumani ajiuzulu

16 Agosti 2023

Upinzani wa siasa kali za mrengo wa kushoto nchini Ujerumani umetumbukia katika msukosuko zaidi baada ya kiongozi wa kundi la wabunge wa chama cha Die Linke, Dietmar Bartsch, kuamua kujiuzulu.

https://p.dw.com/p/4VFjh
Kiongozi wa kundi la wabunge wa chama cha Die Linke Dietmar Bartsch
Kiongozi wa kundi la wabunge wa chama cha Die Linke Dietmar BartschPicha: Mykola Berdnyk/DW

Kiongozi huyo wa muda mrefu mwenye umri wa miaka 65 hatogombea uchaguzi wa ndani ya chama unaopangwa Septemba 4.

Bartsch amesema alifanya uamuzi huo muda mrefu uliopita.

Hivi majuzi, mwenyekiti mwenza Amira Mohamed Ali naye alitangaza kujiondoa, akitaja namna chama kinavyozishughulikia tetesi kuwa kiongozi wake anayefahamika vyema, Sahra Wagenknecht, anaweza kujitoa ili kuanzisha chama kipya.

Kama hilo litatokea, chama cha Die Linke na kundi lake la wabunge katika bunge la taifa, Bundestag, huenda likakumbwa na mpasuko wa ndani ya chama.

Bartsch hata hivyo amesema kujiondoa kwake hakuhusiki na mzozo wa sasa.