1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa upinzani Burundi akamatwa

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Rais wa chama cha upinzani cha Council for Democracy and Sustainable Development nchini Burundi (CODEBU), Kefa Nibizi, anazuiliwa katika gereza kuu la Bujumbura akituhumiwa kwa kuvuruga usalama wa taifa.

https://p.dw.com/p/4XhCT
Symbolbild I Soldaten Burundi
Jeshi la BurundiPicha: Marco Longari/AFP/Getty Images

Mkuu huyo wa chama hicho kidogo cha upinzani nchini Burundi anazuiliwa baada ya kukamatwa siku ya Jumanne (Oktoba 17) kwa kuikosoa serikali kwenye mtandao wa kijamii, kwa mujibu wa afisa wa chama chake na duru ya idara ya mahakama. 

Soma zaidi: Watoto 4 wafa, 15 wajeruhiwa kwa kuangukiwa na kanisa Burundi

Ijumaa iliyopita, chama hicho kilichapisha kauli kuhusu serikali kwenye mtandao wa X, zamani Twitter, wakati wa kumbukumbu ya miaka 62 ya mauaji ya shujaa wa uhuru wa Burundi, Prince Louis Rwagasore.

Katika mfululizo wa taarifa zake, chama kimesikitika kwamba kauli yake haikueleweka kama ilivyonuiwa na kikataka kufafanua ujumbe huo.

Makamu Rais wa CODEBU, Jacqueline Hatungimana, ametoa wito Nibizi aachiwe huru akisema kauli ya chama haihalalishi kuzuiliwa kwake.