1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika UN ziarani Kongo

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2O

Kamishna mkuu anayehusika na masuala ya haki za binadamu katika Umoja wa mataifa Louise Abour ameanza ziara yake ya siku tano nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Katima ziara hii kamishna Abour anatarajiwa kukutana na rais Joseph Kabila na makundi ya kutetea haki za binadamu pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali na wanadiplomasia na mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa William Swing.

Pia amepangiwa kuelekea nchini Burundi na Rwanda kutilia mkazo haja ya kuwepo amani.