1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Watoto mianne waliokua waasi wapokonywa silaha-

25 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFyC

Tume ya umoja wa mataifa iliyopelekwa nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo kusimamia amani, imewapokonya silaha na wakarudishwa katika maisha ya kawaida ya raia, watoto zaidi ya mianne, walioshiriki katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, nchini Kongo-Kinshasa.

Kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa mataifa nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, kwa ushirikiano baina Jumuia hio na Uongozi wa jeshi jipya la Kongo-Kinshasa, wapiganaji wa zamani wa Mai Mai mianane hamsini wamesalimisha silaha zao, wakiwemo watoto mianne kumi na nane.

Msemaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Eliane Nabaa, amesema operesheni ya kupokonya silaha wanamgambo na waasi wa makundi mbali mbali, yaliyozozana katika maeneo tofauti ya nchi hio kubwa, itaendelea-