1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Waasi kunyang’anywa silaha kwa nguvu.

26 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEXb

Jeshi la jamhuri ya kidemokrasi ya Congo limesema jana kuwa litawanyang’anya silaha waasi 400 wa Uganda kwa nguvu , baada ya kuingia katika eneo la kaskazini mashariki ya nchi hiyo na wanakataa kuweka silaha zao chini.

Kamanda wa jeshi la Congo katika jimbo hilo, jenerali Padiri Bulenda , ameliambia shirika la habari la Reuters atalazimika kuwanyang’anya silaha waasi wa Lord Resistance Army LRA ili kuweza kuepusha maelfu ya wanajeshi wa Uganda kuvuka mpaka na kuingia nchini Congo wakiwatafuta waasi hao.

Bulenda amesema amewatembelea waasi hao wenye silaha nyingi siku ya Jumapili.

Serikali ya Congo hapo kabla ilikataa kuwa inafahamu kuwa waasi hao wapo katika nchi hiyo.